22 Septemba 2025 - 19:07
Je, ilikuwa sahihi kutumia vijana baleghe wachanga katika Vita vya Kulazimishwa (Vita vya Iran na Iraq)?

Nchi kadhaa za Ulaya, ikiwemo Ujerumani, zimeruhusu kisheria ajira ya zaidi ya watoto askari 1,500 chini ya utaratibu wa kipekee wa jeshi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-:
Swali linaibuka: Je, kijana mwenye umri wa miaka 13 au 15, ambaye bado hajaruhusiwa na serikali kumiliki leseni ya udereva, anaweza kuruhusiwa kushiriki vitani ambapo uwezekano wa kufa au kupata ulemavu ni mkubwa?. Je, kushirikisha vijana wadogo katika vita hakuhesabiwi kama uhalifu wa kivita?.

1. Fahari ya Jamhuri ya Kiislamu kwa uwepo wa vijana vitani

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijivunii tu kushiriki kwa vijana katika uwanja wa vita, bali fahari yake ni nguvu ya imani, utashi, uelewa na kujitolea kwa vijana hao.

Ushuhuda, mahojiano na wasia wa baadhi ya vijana hawa unaonyesha kiwango cha juu cha ufahamu na uchambuzi wa masuala, kinyume na dhana kwamba walihamasishwa tu kwa hisia.

Kilio na maombi ya vijana hawa kutaka kuruhusiwa kwenda vitani licha ya vizuizi vya makamanda haviwezi kuelezewa tu kama hisia.

2. Msisitizo wa serikali juu ya kutokuwalazimisha vijana

Kinyume na madai ya baadhi ya wakosoaji, serikali ya Iran haikulazimisha wala kusisitiza vijana wachanga washiriki vitani. Kinyume chake, nyaraka zinaonyesha kuwa mara walipotambuliwa, walizuiwa kushiriki mstari wa mbele. Baadhi ya vijana walilazimika hata kughushi vyeti vya kuzaliwa ili kuruhusiwa kujiunga na jeshi, jambo lililokuwa changamoto hata baada ya vita.

Imam Khomeini alikanusha madai ya maadui waliodai watoto walitumwa kwa nguvu vitani. Alisema: “Hakuna mtu anayeruhusiwa kumlazimisha asiye baleghe kwenda vitani. Lakini vijana wa miaka 14 na 15 walikuwa wakikimbia kutoka mikononi mwa wazazi wao na kwenda mstari wa mbele kwa hiari yao.”

3. Uhalifu wa kivita na uhalisia wa Iran

Kwa mujibu wa Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kusajili watoto chini ya miaka 15 ili washiriki moja kwa moja vitani kunahesabiwa kama uhalifu wa kivita.

Lakini hali ya Iran ilikuwa tofauti:

1_Hakukuwa na usajili rasmi au wa kulazimisha kwa watoto wadogo.

2_Waliohudhuria walikuwa kwa hiari yao na mara nyingi walizuiliwa na kurudishwa nyuma.

3_Iran ilitunga sheria ili kuwazuia vijana chini ya miaka 15 kushiriki mstari wa mbele.

Wakosoaji wanaoita hili “uhalifu wa kivita” mara nyingi hupuuzia ukweli huu, huku wakinyamaza pale wanapokutana na mfano wa Ukraine ambapo jeshi linawafundisha watoto mafunzo ya kijeshi bila lawama zozote.

Nchi kadhaa za Ulaya, ikiwemo Ujerumani, zimeruhusu kisheria ajira ya zaidi ya watoto askari 1,500 chini ya utaratibu wa kipekee wa jeshi.

Hitimisho

Kwa kuzingatia ushahidi, Jamhuri ya Kiislamu haikuwahi kulazimisha vijana wadogo washiriki vitani. Mara walipotambuliwa, walizuiwa kwa mujibu wa sheria. Fahari ya Iran ni kwa sababu vijana wake walijitolea kwa hiari na kwa uelewa, si kwa sababu tu ya hamasa ya kihisia.

Uwepo wao vitani ulikuwa ishara ya imani, kujitolea, na uelewa wa hali ya dharura ya kujihami, si sera ya serikali ya kuwasajili watoto kwa nguvu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha